Thursday, March 15, 2012

DAVE RICHARDS SORRY FOR COMMENTS ABOUT UEFA AND FIFA.

MWENYEKITI wa Ligi Kuu nchini Uingereza Sir Dave Richards amelituhumu Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA kuwaibia haki yao ya kuwa nchi ambayo soka liligunduliwa kwa mara ya kwanza. Katika mkutano uliofanyika Qatar Richards ambaye baadae alijiumiza mwenyewe baada yakuteleza kwenye ngazi amesema kuwa dunia inabidi iishukuru nchi ya Uingereza kwa kuanzisha mchezo huo. Richards aliendelea kusema kuwa nchi ndio iliwapa dunia mchezo wa mpira lakini miaka 50 baadae mtu anakuja kusema kuwa ni uongo na kutunyang’anya haki hiyo ambapo alidai mtu huyo ni FIFA. Richards ambaye ni mjumbe wa bodi ya Chama cha Soka nchini Uingereza-FA alizungumza hayo mbele ya Makamu wa Rais wa FIFA Ali Bin Hussein wa Jordan na Ofisa Mkuu wa Baraza la Kimatifa la Kriketi Haroon Lorgat. Kauli ya Richards imekuja wakati wa mapendekezo yaliyotolewa kuwa mchezo wa soka umeanzia nchini China. Richards amesema kuwa mchezo wa soka umeanzia katika kitongoji cha Shiffield miaka 150 iliyopita na Uingereza ndio iliyoandika sheria na kuzitoa duniani kote hivyo hadhani kama ni halali China kupewa haki hiyo. Kauli ambayo baadae aliomba msamaha kutokana na kauli yake hiyo.

No comments:

Post a Comment