Saturday, March 10, 2012
GHANA SPORTS MINISTRY WON'T PAY PLAVI.
MJADALA kuhusu malipo ya kocha wa timu ya taifa ya Ghana-Black Stars, Goran Stevanovic umeendelea ambapo Wizara ya Vijana na Michezo ya nchi hiyo imejitoa kumlipa kocha huyo huyo kama wakiamua kusitisha mkataba wake. Maamuzi kuhusiana na uwepo wa kocha huyo yatatangazwa wiki ijayo baada ya mkutano wa mwisho wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la nchi hiyo-GFA na kocha huyo lakini watalazimika kumlipa kiasi cha Euro 135,000 kama wakiamua kusitisha mkataba wake kiasi ambacho itabidi kitoke katika vyanzo vingine na sio Wizarani. Gazeti moja la habari za michezo nchini humo limeandika kuwa Wizara imefurahishwa kuondolewa kuhusiana na suala la kocha huyo na ipo pamoja na GFA kwa maamuzi watakayochukua. Hatahivyo pamoja na fedha nyingi ambazo zimetumika kwa ajili timu hiyo na nyingine ambazo zitaendelea kutumika kwa ajili ya michezo ya kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Kombe la Afrika 2013 na Kombe la Dunia 2014 wizara haitakuwa kuwa tayari kuingia gharama zaidi. Pia wizara hiyo ndio inayomlipa kocha huyo raia wa Serbia kiasi cha dola 45,000 kwa mwezi hivyo GFA lazima itafute pesa kutoka chanzo kingine ili waweze kumlipa kocha huyo kama watamtimua.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment