Sunday, March 11, 2012

LIGI KUU NCHINI MISRI YAFUTWA.

CHAMA cha Soka chini Misri-EFA kimesitisha kabisa Ligi Kuu ya nchini humo kufuatia vurugu zilizopelekea watu 74 kupoteza maisha katika moja ya michezo ya michezo ya ligi hiyo na wengine mamia kuumia. Ligi hiyo ilisimamishwa baada ya tukio hilo ambalo lilitokea Februari 1 mwaka huu wakati wa mchezo wa baina ya Al Ahly na Al Masry uliofanyika huko Port Said. Msemaji wa EFA Azmy Megahed amesema ligi hiyo haiwezi kuendelea tena msimu huu kwasababu hakutakuwa na muda wa kutosha kucheza mechi zilizobakia kabla ya timu ya taifa ya nchi hiyo haijaanza mazoezi kwa ajili ya michuano ya Olimpiki pamoja na kutafuta tiketi ya kucheza Kombe la Mataifa ya Afrika 2013. Lakini Megahed amesema timu 18 zitachuana katika mashindano ambayo yatakuwa ya hisani huku viwanja vikiwa vitupu ili kukusanya fedha kwa ajili familia ambazo zilipoteza ndugu zao katika vurugu hizo.

No comments:

Post a Comment