Wednesday, March 21, 2012

MESSI, FROM SCRAWNY KID TO WORLD'S BEST.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka Argentina Lionel Messi amefanikiwa kuwa mfungaji bora wa kihistoria wa klabu ya Barcelona baada ya kuisaidia timu hiyo kushinda mabao 5-3 katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania dhidi Granada huku yeye akifunga mabao matatu-hat trick katika mchezo huo. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo meneja wa timu hiyo Pep Guardiola amesema kuwa mchezaji huyo anastahili kila kitu ambacho mwanasoka anatakiwa kuwa nacho na amefanya hivyo kila baada ya siku tatu kwa kuonyesha kiwango cha kipekee. Messi ambaye katika mchezo alifunga hat trick yake ya 18 toka aanze kuichezea klabu hiyo na kupelekea kuvunja rekodi ya nyota wa zamani wa klabu hiyo Cecar Rodriguez aliyefunga mabao 232 rekodi ambayo imedumu kwa muda wa miaka 57. 
Wakati Rodriguez akiweka rekodi hiyo ndani ya miaka 13 kuanzia mwaka 1942 mpaka 1955, Messi ambaye ana umri wa miaka 24 sasa ametumia misimu nane tu aliyochezea Barcelona kuvunja rekodi hiyo. Messi ambaye pia ni mwanasoka bora wa dunia mara tatu mfululizo sasa amefikisha mabao 54 kwenye mashindano yote aliyocheza msimu huu yakiwemo mabao matano aliyoshinda na kuweka rekodi nyingine katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki mbili zilizopita ambapo kwasasa amemzidi hasimu wake Cristiano Ronaldo mabao mawili.

No comments:

Post a Comment