MUAMBA AIZINDUA FIFA.
|
Jiri Dvorak. |
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa-FIFA, inafanya uchunguzi juu ya matatizo ya moyo yanayowakumba wachezaji ili kubaini kiini cha matatizo hayo. Hatua hiyo inafuatia kiungo mwenye asili ya DRC, Fabrice Muamba kuanguka uwanjani na kuzimia na hadi sasa amelazwa, ingawa ameanza kupata nafuu. Ofisa Mkuu wa Tiba wa FIFA, Jiri Dvorak, amesema leo kwamba mpango huo utafanyika katika mkutano wa tiba Mei 23 na 24 mjini Budapest, Hungary. Dvorak amesema kuwa katika mkutano wamewaalika madokta wote wa timu za taifa ili kuangalia kwa kina matatizo hayo ya moyo yanayowakumba wachezaji. Kwasasa Muamba mwenye miaka 23 hali yake inaendelea vizuri ingawa bado yuko katika uangalizi maalumu katika hospitali ya London Chest nchini Uingereza ambapo amelazwa toka alipoanguka wakati wa mchezo war obo fainali ya Kombe la FA.
No comments:
Post a Comment