Tuesday, March 27, 2012

REAL MADRID, CHELSEA KIBARUANI ULAYA LEO.

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya inaendelea tena leo ambapo viwanja viwili vitawaka moto katika michezo ya robo fainali ya michuano hiyo. Katika michezo ya leo timu ya APOEL Nicosia itakuwa na kibarua kigumu wakati itapoikaribisha timu ya Real Madrid katika wake wa nyumbani nchini Ugiriki huku wpinzani wao hao wakipewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo. Kocha wa Madrid Jose Mourinho amewatahadharisha wachezaji wake kuwa mchezo huo hautakuwa rahisi hivyo wajizatiti na kucheza katika kiwango chao cha juu baada ya siku za hivi karibuni kuonekana wakilegalega katika Ligi Kuu nchini Hispania kwa kupoteza baadhi ya pointi. Mchezo mwingine ambao nao unatarajiwa kuwa mgumu utakuwa ni kati ya Benfica ya Ureno ambao wataikaribisha Chelsea katika uwanja wao wa nyumbani ambapo ushindi wataoupata katika mchezo huu wa kwanza utawaweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele. Chelsea itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuitoa Napoli kwa ushindi wa kushangaza chini ya kocha wake Roberto Di Matteo ambaye toka alipoanza kuinoa klabu hiyo imeonekana kurudi kwenye kiwango kizuri licha ya kufungwa na Manchester City katika mchezo wa LIgi Kuu nchini Uingereza.

No comments:

Post a Comment