Thursday, March 22, 2012

MUAMBA ALIKUFA KWA DAKIKA 78-DAKTARI.

Dr Jonathan Tobin
DAKTARI wa klabu ya Bolton Wanderers Jonathan Tobin amebainisha kuwa mchezaji wa klabu hiyo Fabrice Muamba katika dakika 78 toka alipozirai uwanjani ni kama likuwa amekufa. Jopo la madaktari wanaomtibu mchezaji huyo katika Hospitali ya London Chest nchini Uingereza wamesema kuwa kwasasa bado ni mapema mno kutabiri kama ataweza kucheza soka tena. Lakini Tobin amesema kuwa ameshangazwa na jinsi mchezaji mwenye umri wa miaka 23 alivyoweza kupata nafuu mpaka muda huu. Akihojiwa kwa masikitiko Tobin aliendelea kusema kuwa wao wenyewe hawakutegemea kama mchezaji huyo anaweza kupata nafuu kama aliyonayo sasa kwani fikra zao zilikuwa zimewaza mengine kabisa. Amesema kuwa walijitahidi kuinua moyo wa Muamba ili ufanye kazi mara moja uwanjani na mara nyingine wakati akipelekwa katika gari la wagonjwa na akiwa katika gari hilo walijaribu karibu mara 12 lakini hawakufanikiwa kuustua moyo wake. Moyo wa Muamba ulianza kufanya kazi akiwa hospitalini baada ya dakika 78 toka usimame kufanya kazi hivyo ni kama maajabu lakini jambo muhimu ni jinsi alivyopata huduma ya kwanza mara tu alipoanguka uwanjani na kuzirai na majaribio yaliokuwa yakifanywa kuamsha moyo wake.

No comments:

Post a Comment