Thursday, March 22, 2012

"CARDIAC ARREST" YAMUUA MCHEZAJI INDIA.

Baadhi ya wachezaji na watu wa huduma ya kwanza wakimbeba D Venkatesh ili kumuwahisha hospitalini.
MCHEZA soka nchini India amefariki dunia baada ya kuanguka na kuzirai wakati akicheza mpira ikiwa ni siku chache baada ya mchezaji wa Bolton Wanderers Fabrice Muamba kukumbwa na tatizo kama hilo katika mchezo wa Kombe la FA nchini Uingereza Jumamosi iliyopita. Mchezaji huyo anayeitwa D Venkatesh mwenye umri wa miaka 28 alianguka baada ya moyo wake kusimama kufanya kazi ikiwa ni muda mfupi baada ya kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba wakati wa mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati ya timu yake ya Bangalore Mars dhidi ya South Western Railway. Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa hakukuwa na na gari la wagonjwa uwanjani hapo wakati tukio hilo lilikitokea hivyo kupelekea mchezaji huyo kukimbizwa hospitali na pikipiki za miguu mitatu maarufu kama Bajaj. Taarifa hiyo pia ilithibitishwa na Shrikisho la Soka nchini India-AIFF juu ya kifo cha mchezaji huyo ambaye alifariki wakati akifikishwa hospitalini.

No comments:

Post a Comment