Friday, March 16, 2012

PIQUE AFUTIWA MASHTAKA.

MAMLAKA ya Soka nchini Hispania imeamua kufunga mjadala wa malalamiko ya kamati ya waamuzi dhidi ya beki wa Barcelona Gerrard Pique wakimtuhumu kumshambulia mwamuzi baada ya kumpa kadi nyekundu. Taarifa iliyotolewa na mmoja wa viongozi wa shirikisho hilo imesema kuwa Kamati ya Mashindano imeamua kufunga mjadala huo wa kamati wa waamuzi dhidi ya Pique. Shirikisho hilo tayari limemfungia mchezaji huyo mchezo mmoja na faini ya euro 600 baada yak umjia juu mwamuzi katika mchezo baina ya timu yake na Sporting Gijon uliochezwa Machi 13 mwaka huu. Kamati hiyo inayowakilisha waamuzi ilitoa malalamiko yao kuhusu kauli ya Pique akimlenga mwamuzi Velasco Carballo ambaye alichezesha mchezo huo ambapo timu yake Barcelona ilituma barua ya kumtete mchezaji huyo kupinga kuwa mchezaji huyo alimdhalilisha mwamuzi. Pique alitolewa nje baada ya kumchezea vibaya Miguel De Las Cuevas dakika ya 47 mchezo ambao Barcelona ilishinda kwa mabao 3-1 dhidi Gijon.

No comments:

Post a Comment