Tuesday, March 20, 2012

TAARIFA MBALIMBALI KUTOKA TFF.

MKUTANO MKUU TFF APRILI 21
Mkutano Mkuu wa kawaida wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) uliokuwa ufanyike Machi 24 na 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam umesogezwa mbele hadi Aprili 21 na 22 mwaka huu. Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Machi 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam chini ya uenyekiti wa Rais Leodegar Tenga uliamua kusogeza mbele Mkutano Mkuu kutokana na mtiririko wa matukio ndani ya TFF katika kipindi hicho. Ajenda katika Mkutano Mkuu huo wa kawaida wa TFF kufungua kikao, kuthibitishwa kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu, kuthibitisha muhtasari wa Mkutano Mkuu uliopita, yatokanayo na muhtasari wa kikao kilichopita, hotuba ya Rais, kupokea taarifa za utekelezaji za wanachama na kupokea taarifa ya utekelezaji ya Kamati ya Utendaji. Nyingine ni kupitisha taarifa ya ukaguzi wa hesabu za mwaka uliopita, kupitisha taarifa ya wakaguzi wa hesabu na hatua zilizochukuliwa, kupitisha bajeti ya mwaka 2012, kupitisha mapendekezo ya marekebisho ya Katiba ya TFF, kujadili mapendekezo yaliyowasilishwa na Wanachama au Kamati ya Utendaji, mengineo na kufunga kikao.

MTIBWA SUGAR, SIMBA ZAINGIZA MIL 31/-

Mechi namba 146 ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Mtibwa Sugar na Simba iliyochezwa Machi 18 mwaka huu Uwanja wa Jamhuri, Morogoro imeingiza sh. 31,230,000. Jumla ya watazamaji 10,410 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 3,000. Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ambayo ni sh. 4,763,898.31 kila timu ilipata sh. 6,508,230.51, uwanja sh. 2,169,410.17.  Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) sh. 867,764.07, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 2,169,410.17, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 1,084,705.08, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 216,941.02 na asilimia 10 ya gharama za mechi sh. 2,169,410.17. Gharama za awali za mechi zilikuwa nauli ya ndani kwa waamuzi sh. 10,000, nauli ya ndani kwa kamishna wa mchezo sh. 10,000. mwamuzi wa akiba sh. 30,000, posho ya kujikimu kwa waamuzi sh. 120,000 na tiketi sh. 2,480,000.  Gharama nyingine ni Jichangie ambayo ni sh. 200 kwa kila tiketi; kila klabu ilipata sh. 728,700 wakati Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Morogoro (MRFA) kilipata sh. 624,600.

VILLA, JKT KUHITIMISHA RAUNDI YA 21 MACHI 21

Mzunguko wa 21 wa Ligi Kuu ya Vodacom unakamilika Machi 21 mwaka huu kwa mechi namba 147 kati ya Villa Squad na JKT Ruvu itakayochezwa Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Machi 24 mwaka huu kutakuwa na mechi ya ligi hiyo kati ya Moro United na African Lyon. Mechi hiyo namba 149 itafanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam. Mechi za Machi 28 mwaka huu ni Ruvu Shooting Stars itakayocheza na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi wakati Moro United itakuwa mwenyeji wa Villa Squad katika mechi namba 153 itakayofanyika Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam.

35 ES SETIF KUWASILI MACHI 21

Kikosi cha watu 35 cha timu ya ES Setif ya Algeria kinatarajiwa kuwasili nchini kesho (Machi 21 mwaka huu) saa 12 alfajiri kwa ndege ya EgyptAir kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Simba itakayochezwa Machi 25 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Msafara huo una wachezaji, benchi la ufundi, viongozi wa timu, kiongozi wa msafara kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu la Algeria (FAF) wakati watatu ni waandishi wa habari. Wachezaji 20 katika msafara huo ni Mohamed Benhamou, Sofiane Bengorine, Riadh Benchadi, Smain Diss, Farouk Belkaid, Khaled Gourmi, Mourad Delhoum, Said Arroussi, Mokhtar Benmoussa, Tarek Berguiga, Mohamed Aoudi na Amir Karaoui. Wengine ni Mohamed El Amine Tiouli, Racid Ferrahi, Youcef Ghezzali, Youssef Sofiane, Mokhtar Megueni, Rachid Nadji, Abderrahmane Hachoud na Akram Djahnit. Kocha wa timu hiyo ni Alain Norbert Geiger ambaye ni raia wa Uswisi.




No comments:

Post a Comment