Tuesday, March 20, 2012

MESSI KINARA WACHEZAJI WANAOLIPWA ZAIDI DUNIANI.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Barcelona Lionel Messi ndiye mchezaji wa mpira anayelipwa zaidi duniani akifuatiwa na David Beckham wa Uingereza na Cristiano Ronaldo wa Ureno. Messi ambaye anacheza katika klabu ya Barcelona anakunja kitita cha euro milioni 33 ikiwemo euro milioni 10.5 za mshahara wake, euro milioni 1.5 kama motisha na euro milioni 21 za matangazo na mikataba mingine. Kiungo wa zamani wa Manchester United ambaye kwasasa anakipiga katika klabu ya Los Angeles Galaxy ya Marekani, David Beckham anakunja kitita cha euro milioni 31.5 sehemu kubwa ya fedha hizo ambazo ni kiasi cha euro milioni 26 za matangazo na mikataba mbalimbali ambayo amesaini. Ronaldo ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid anashika nafasi ya tatu katika orodha orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi kwa kujikusanyia kiasi cha euro 29.2, ambapo euro milioni 13 ni za mshahara wake kwa mwaka na euro milioni 15.5 ni matangazo na mikataba mingine mbalimbali.

No comments:

Post a Comment