Tuesday, March 20, 2012

WAJUE MAKOCHA WANAOLIPWA PESA NYINGI ZAIDI DUNIANI.

MENEJA wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho ndiye kocha anayelipwa hela nyingi zaidi duniani kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na gazeti moja la michezo nchini Ufaransa. Mourinho ambaye pia amewahi kuinoa klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza kwa mwaka anakusanya kiasi cha euro milioni 14.8 wakati makocha wawili ambao nao pia wamewahi kuinoa Chelsea pia wamo katika orodha hiyo. Katika orodha hiyo Carlo Ancelotti ambaye anainoa klabu ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa ndiye anashika nafasi ya pili katika makocha wanaolipwa zaidi akikunja kiasi cha euro milioni 13.5 kwa mwaka akifuatiwa na Pep Guardiola katika nafasi ya tatu akikunja kiasi cha euro 9.5. 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ndiye anashika nafasi ya nne katika orodha hiyo akipokea kiasi cha euro milioni tisa akifuatiwa na Guus Hiddink ambaye kwasasa anakinoa kikosi cha Anzhi Makhachkala yeye anapokea euro 8.6 kwa mwaka. Wengine ni meneja wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza Fabio Capello ambaye anaweka kibindoni kiasi cha euro milioni 8.5 akifuatiwa na Sir Alex Ferguson ambaye anakunja kitita cha euro milioni nane. Pia wapo Dick Advocaat kocha timu ya taifa ya Urusi euro milioni saba, Antonio Camacho kocha timu ya taifa ya China euro milioni 6.1 na orodha hiyo inafungwa na kocha wa Manchester City Roberto Mancini ambaye anakunja kitita cha euro milioni 5.9.

No comments:

Post a Comment