Tuesday, March 20, 2012

MUAMBA AANZA KUTAMBUA NDUGU.

KIUNGO wa klabu ya Bolton Wanderers Fabrice Muamba ameanza kupumua bila kutumia msaada wa mashine na ameanza kutambua baadhi ya watu wa karibu wa familia yake hivyo kuonyesha dalili za kupona baada ya moyo wake kushindwa kufanya kazi ghafla Jumamosi. Kiungo huyo huyo wa kimatiga kutoka Congo ambaye ana umri wa miaka 23 alianguka uwanjani muda kidogo kabla ya mapumziko wakati wa mchezo baina ya timu yake na Tottenham Hotspurs ambapo juhudi za kuuzindua moyo wake hapo uwanjani zilishindikana na kupelekea kukimbizwa hospitalini. Kwa mujibu wa taarifa ya madaktari moyo wa Muamba ulianza kufanyakazi baadae akiwa hospitalini hapo na kuendelea kuwekwa chini ya uangalizi maalumu huku akitumia mashine za kumsaidia kupumua kwa muda wa siku mbili. Lakini mchezaji huyo hali yake iliendelea vizuri hadi jana ambapo madaktari wanaomtibu wamesema kuwa hali yake imetengemaa ilipofika jana jioni lakini bado ataendelea kuwepo hospitalini hapo mpaka hapo madaktari watapojiridhisha kwamba amepona kabisa. Mchumba wa mchezaji huyo ambaye alimchumbia wakati wa sherehe za wapendanao Februari mwaka huu aitwae Shauna Muamba amewashukuru watu wote waliokuwa wakimuombea mchumba wake huyo kwani maombi yao yamesikilizwa, aliandika Shauna katika mtandao wa kijamii wa twitter.

No comments:

Post a Comment