Thursday, March 8, 2012

ZAMALEK, AL AHLY KUCHEZA MCHEZO WA HISANI KUWAKUMBUKA WALIOPOTEZA MAISHA.

MWENYEKITI wa klabu ya Zamalek, Mamdouh Abbas ametangaza kwamba mechi ijayo dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Al Ahly itafanyika baadaye mwezi huu. Abbas ameaimbia SuperSport kwamba amekubaliana na Mwenyekiti wa Al Ahly, Hassan Hamdy na ofa hiyo imekubaliwa, sasa wanasubiria Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi hiyo kuwaunga mkono ili kuidhinisha mchezo huo ambao wamepanga ufanyike Machi 23 au 27 mwaka huu. Abbas amesema kuwa katika mchezo huo, kila timu itavaa jezi za mpinzani wake ili kuonyesha umoja, hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya upinzani wa timu hizo. Mechi hii inakuja siku chache baada ya kutokea janga la mauaji ya watu 74 lililotokea kwenye mji wa Port Said wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Misri kati ya Al Masry na Al Ahly.

No comments:

Post a Comment