Saturday, March 10, 2012

DROGBA KUCHANGISHA ZA MFUKO WAKE.

MFUKO wa Didier Drogba, leo utafanya hafla ya uchangishaji fedha katika hoteli ya Dorchester Hotel mjini London, lengo likiwa ni kukusanya kiasi cha pauni Milioni 3 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa hospitali nchini kwao Ivory Coast. Zoezi hilo la tatu kufanyika katika mradi huo, linatarajiwa kuhusisha watu kibao maarufu, wakiwemo wanasoka nyota duniani na wanasiasa. Mazagazaga kibao, zikiwemo jezi za mchezaji huyo, za rafiki zake na wachezaji wenzake, viatu, soksi na kadhalika vitauzwa kwenye zoezi hilo la hisani. Nahodha huyo wa kimataifa wa Ivory Coast amesema kuwa ushirikiano ambao amepata katika mfuko wake huo ni kubwa na akasisitiza kuwa bado wana kazi kubwa huko ya kufanya katika siku zijazo. Kituo cha afya cha Gigantic kinajengwa katika wilaya ya Attecoube mjini Abidjan, eneo la watu fukara ambalo linakosa hadi zana za kisasa za tiba na huduma hospitalini hapo zitakuwa zikitolewa bure.

Mfuko huo uitwao-Didier Drogba Foundation ulianzishwa mwaka 2007, kwa lengo la kushughulika na masuala ya kiafya na elimu Afrika.

No comments:

Post a Comment