Saturday, March 10, 2012

FIFA WAAHIRISHA SAFARI YA BRAZIL.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA wameahirisha ziara yao ya kwenda kukagua maendeleo ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 kutokana na kauli aliyotoa Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Jerome Valcke kuhusu ucheleweshwaji wa maandalizi hayo. Rais wa FIFA Sepp Blatter ndio atakuwa wa kwanza kwenda nchini Brazil kukutana na Rais wa nchi hiyo Dilma Rousseff, mkutano ambao unatarajiwa kuwepo wiki ijayo kwa mujibu wa taarifa iliyotolea na mtandao wa FIFA. Valcke anatarajiwa kutua nchini humo baada ya mkutano huo baina ya Blatter na Rousseff ambapo atajiunga na mshambuliaji wa zamani nyota wan chi hiyo Ronaldo na Bebeto ambao ni wajumbe katika kamati ya maandalizi katika michuano hiyo kutembelea miji ya Recife, Brasilia na Cuiaba. Valcke alitoa kauli akiwataka Brazil kujituma zaidi katika maandalizi hayo akidai kuwa wako nyuma kauli ambayo Waziri wa Michezo wan chi hiyo Aldo Rebelo hakuridhishwa nayo akidai kuwa ni kudhalilisha na kuudhi hiyo hawataki kufanya kazi na katibu huyo kwenye maandalizi hayo kabla ya Valcke na Blatter kuomba msamaha baadae.

No comments:

Post a Comment