Friday, April 20, 2012

BECKHAM HASTAHILI KUITWA UINGEREZA-LINEKER

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Uingereza Gary Lineker amesema kuwa David Beckham hastahili nafasi katika kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki michuano ya Olimpiki baadae mwaka huu. Kocha wa timu ya taifa ya nchi hiyo Stuart Pearce anaweza kuchagua wachezaji watatu wenye umri mkubwa ili kuongeza nguvu katika kikosi chake cha vijana chini ya miaka 23. Akinukuliwa Lineker amesema kuwa kama unatakiwa kuchagua majina matatu ya wachezaji ambao wamevuka umri sidhani kama Beckham atakuwa mmojawapo. Mshambuliaji huyo wa zamani wan chi hiyo pia alitoa wito kwa Chama cha Soka cha nchi hiyo-FA kuteua kocha mapema atakayekinoa kikosi hicho kabla ya michauno ya Olimpiki. Beckham ambaye ni nahodha wa zamani wa Uingereza ni mmoja kati ya wachezaji 80 ambao wako katika kinyang’anyiro cha kugombania nafasi katika kikosi hicho na ameonyesha nia ya kukiongoza kikosi hicho katika michuano hiyo itakayofanyika jijini London.



No comments:

Post a Comment