Tuesday, April 17, 2012

BLANC MGUU NJE MGUU NDANI UFARANSA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Ufaransa Laurent Blanc huenda akarudi kufundisha katika vilabu kutokana na Shirikisho la nchi hiyo kutomuongeza mkataba mwingine kocha huyo. Blanc amekuwa akihusishwa kwenda kufundisha katika Ligi Kuu ya Uingereza au Italia ambapo vilabu vya Chelsea na Inter Milan vimeripotiwa kuhitaji huduma ya kocha huyo. Gazeti moja nchini Ufaransa lilimnukuu kocha huyo akisema kuwa kibarua chake cha kuinoa timu hiyo kinakaribia kufikia mwishoni kwani hajui msimu ujao atakuwa akifanya shughuli gani. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Blanc amesema kuwa huwa anafurahishwa na vilabu vikubwa vinapogombania saini yake lakini akasisitiza kuwa mawazo yake kwasasa yapo katika michuano ya Kombe la Ulaya ambayo inatarajiwa kuanza Juni 8 huko Poland na Ukraine. Hata hivyo Blanc aliweka angalizo kuwa atakuwa tayari kuondoka kama vilabu hivyo vinavyomuhitaji vitampatia fungu la kueleweka.

No comments:

Post a Comment