Thursday, April 19, 2012

'CLASICO' HIGH NOON FOR RONALDO AND MESSI.

PAMOJA na kupoteza michezo yao katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu za Barcelona na Real Madrid zinatarajiwa kujitupa uwanjani katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga. Madrid watakwenda Nou Camp huku wakiwa wanaongoza ligi hiyo kwa alama nne zaidi ya mahasimu wao Barcelona huku washambuliaji wake nyota Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wakiwa tayari wamefunga mabao 41 msimu huu pekee. Ronaldo ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ureno, msimu uliopita alifanikiwa kuweka rekodi ya kushinda mabao 40 ambapo mpaka sasa ameshafunga mabao 53 katika mashindano yote wakati Messi ambaye ni raia wa Argentina ameshafunga mabao 63 katika mashindano yote yakiwemo 14 katika michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya. Messi mpaka sasa yuko nyuma kwa mabao manne kufikia rekodi ya mabao 67 iliyowekwa na mshambuliaji wa Bayern Munich Gerd Mueller katika msimu wa mwaka 1972-1973.

No comments:

Post a Comment