Thursday, April 19, 2012

CHINESE CLUB DENIES HIRING LIPPI.

Marcelo Lippi
KLABU ya Guangzhou Everngrade ya nchini China ambayo inasifika kwa matumizi makubwa katika usajili wa wachezaji nyota, imekana kumsajili kocha Marcelo Lippi kutoka Italia kwa mkataba wa mamilioni ya dola. Katika kipindi cha karibuni magazeti mbalimbali nchini humo yamekuwa yakiandika habari kuhusiana na kocha huyo kujiunga na klabu hiyo tajiri kwa mkataba mnono wa kiasi cha dola milioni 23. Rais wa klabu hiyo Liu Yongzhuo ameonyesha kumuamini kocha wa sasa wa klabu hiyo Lee Jang-Soo kutoka Korea Kusini ambaye amekiongoza kikosi cha Everngrade baada ya kuiwezesha kushinda taji la Ligi Kuu nchini humo msimu uliopita ingawa hakuonekana kupinga suala la uhamisho wa Lippi. Lippi ambaye amewahi kuzinoa klabu za Inter Milan, Juventus pamoja na klabu zingine kubwa nchini Italia alikaririwa akikana tetesi hizo na kusema kuiwa hazina ukweli wowote.

No comments:

Post a Comment