Tuesday, April 17, 2012

HATUJALI HISTORIA-MOURINHO

KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amesisitiza kuwa historia haitakuwa na nafasi wakati kikosi chake kitapojitupa uwanjani kumenyana na Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Katika mara tisa ambazo Madrid na Bayern wamecheza jijini Munich, Wajerumani hao wameweka rekodi ya kushinda michezo nane na kutoa suluhu mmoja katika michuano hiyo mikubwa ya vilabu barani Ulaya toka mwaka 1976. Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana katika michuano hiyo ya Ligi ya mabingwa miaka mitano iliyopita Bayern walishinda katika hatua ya timu 16 kwa bao la ugenini baada ya kufungana bao 4-4 katika michezo miwili waliocheza ambapo katika mchezo wa kwanza Bayern walishinda mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Madrid huku na wao pia wakishinda mabao 3-2 huko Hispania. Lakini Mourinho amesema kuwa rekodi hiyo haina maana yoyote wakati kikosi chake kitapotua jijini Munich leo kupambana na Bayern huku wakiwa tayari wamefunga mabao 107 katika Ligi Kuu nchini Hispania na nyota wake Cristiano ronaldo akiwa amefunga mabao 41 kati ya hayo.

No comments:

Post a Comment