Wednesday, April 4, 2012
NESTA BEMUSED BY PENALTY DECISION.
BEKI wa AC Milan, Alessandro Nesta amesema kwamba penati iliyotolewa kwa sababu yake usiku wa jana katika mchezo robo fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Barcelona haikuwa halali. Mwamuzi Bjorn Kuipers ambaye alichezesha mchezo huo aliamuru penati baada ya beki huyo wa zamani wa kimataifa wa Italia kuwafanyia madhambi wachezaji wa Barcelona Carles Puyol na Sergio Busquets katika eneo la hatari wakati wakisubiri mpira wa kona kabla ya mapumziko. Milan ilikerwa na uamuzi huo, kutoa adhabu wakati mpira haujachezwa wakati huo, na Nesta amesema kwamba hajui kwa nini ilitolewa ile penati. Pamoja na kulalamikia penati hiyo Nesta amekiri kuwa timu yake imefungwa na timu bora na anaamini kwamba watajipanga ili msimu ujao aje kwa nguvu zaidi na kusongea mbele zaidi katika mashindano hayo. Barcelona sasa inasubiri mshindi kati ya Benfica au Chelsea katika mchezo wa robo fainali nyingine itakayochezwa leo wakati Bayern Munich ambao nao jana walifanikiwa kuingia nusu fainali kwa kuitoa Olympique Marseille, watasubiri kucheza na mshindi kati ya Real Madrid au APOEL Nicosia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment