Wednesday, April 4, 2012

TRAORE ASHINDA KESI.

ALIYEKUWA kocha wa timu ya taifa ya Senegal Amara Traore jana amefanikiwa kushinda kesi yake dhidi ya Shrikisho la Soka la nchi hiyo-FSF na atatakiwa kulipwa kiasi cha dola 560,000 zikiwa ni pesa zake za mshahara wa miezi miwili pamoja na posho za likizo. Mahakama ya Saint Louis iliyopo jijini Dakar ilimpa ushindi kwenye kesi hiyo mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wan chi hiyo ambaye ana umri wa miaka 49 baada ya kuwasilisha malalamiko mawili katika makahama hiyo moja likiwa ni kufukuzwa kwa kudhalilishwa na lingine akidai malipo yake. Mahakama hiyo pia imesema itatoa hukumu April 10 mwaka huu kwa shitaka la pili lililowakilishwa na Amara kuhusu kutotendewa haki wakati akitimuliwa kibarua chake. Wakili wa FSF Ndiaga Dabo ameuelezea uamuzi huo kama wa kushangaza na ameahidi kukata rufani kupinga uamuzi huo wa mahakama.

No comments:

Post a Comment