Thursday, May 24, 2012

DOHA, BAKU ZATOLEWA KUANDAA OLIMPIKI 2020.

MIJI ya Istanbul, Uturuki, Tokyo, Japan na Madrid, Hispania ndio miji pekee iliyobaki katika kinyang’anyiro cha kugombea kuwa mwenjeji wa michuano ya Olimpiki na Olimpiki kwa walemavu-Paralympics baada ya miji ya Doha, Qatar na Baku, Azerbaijan kutolewa katika kinyang’anyiro hicho jana. Orodha ya miji iliyobakia kuwania kuandaa michuano hiyo 2020 ilitangazwa katika mkutano wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, mkutano ambao ulifanyika jijini Quebec, Canada. Miji ya Doha na Baku imeondolewa katika kinyang’anyiro hicho kwa mara ya pili baada ya kushindwa kufika kwenye orodha ya mwisho kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo kwa mwaka 2016. Bodi ya maofisa yenye wajumbe 15 wakiongozwa na rais wa IOC Jacques Rogge walichagua orodha hiyo ya mwisho baada ya kupewa taarifa ya usaili iliyofanywa jopo la wataalamu wa Olimpiki, ambapo nchi itakayopewa ridhaa ya kuandaa michuano hiyo itatangazwa Septemba 7 mwaka 2013 jijini Buenos Aire, Argentina. Mji wa Tokyo uliandaa michuano ya Olimpiki mwaka 1964 wakati Istanbul na Madrid yenyewe bado haijawahi kuandaa michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment