Saturday, May 19, 2012

HAVELANGE KURUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI.


Joao Havelange




MADAKTARI wanaomtibu rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Joao Havelange wamesema kuwa rais huyo ambaye amelazwa hosptitalini hapo kwa zaidi ya miezi miwili baada ya kupata maambukizi ya bacteria katika mguu wake wa kulia anatarajiwa kuruhusiwa. Taarifa kutoka katika Hospitali ya Samaritano ambako amelazwa Havelange inasema kuwa anaendelea vizuri baada ya kutolewa chumba chenye uangalizi maalumu wiki iliyopita ambapo baada ya siku chache anatarajiwa kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya madaktari kujiridhisha kama hali yake imetengemaa kabisa. Havelange ambaye ana umri wa miaka 96 alilazwa hospitalini hapo Machi 18 mwaka huu baada ya kupata maambukizi ya bacteria ambao walikuwa wakishambulia maungio ya mguu wake wa kulia na baadae hali yake kubadilika baada ya kusumbuliwa na moyo pamoja na kushindwa kupumua sawasawa. Mzee huyo aliiongoza FIFA kuanzia mwaka 1974 mpaka 1998 alipomwachia madaraka rais wa sasa Sepp Blatter na anabakia kuwa rais wa heshima wa shirikisho hilo ambapo pia mwaka jana alijiuzulu wadhifa wa Ujumbe wa Kamati wa Kimataifa ya Olimpiki kutokana na matatizo ya kiafya.

No comments:

Post a Comment