MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi na wachezaji wa Manchester City ambao ndio mabingwa wa Ligi Kuu nchini Uingereza wametajwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Argentina kwa ajili ya mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador utakaofanyika June 2 mwaka huu. Mbali na mchezo huo Argentina pia inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki na timu ya taifa ya Brazil utakaofanyika June 9 nchini Marekani. Kikosi hicho ambacho kinanolewa na kocha Alejandro Sabella kinaonekana hakina mabadiliko makubwa zaidi ya kumuita kwa mara ya kwanza beki wa timu ya Universidad ya Chile Matias Rodriguez. Uruguay ndio wanaongoza katika msimamo wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia kwa timu za Amerika Kusini wakiwa na alama saba kutokana na michezo mitatu waliyocheza wakifuatiwa na Argentina na Venezuela ambao wote wana alama saba katika michezo minne waliyocheza.
Saturday, May 19, 2012
MESSI, AGUERO, ZABALETA WAITWA KIKOSI CHA ARGENTINA.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment