Friday, May 11, 2012

HAWK-EYE KUJARIBIWA UINGEREZA.

MAJARIBIO ya awamu ya pili ya mfumo wa teknologia ya kompyuta kwenye mstari wa goli uitwao Hawk-Eye imeanza ikiwa imebaki miezi miwili kabla Bodi ya Kimataifa ya mchezo wa Soka-IFAB haijaamua kama teknologia hiyo itumike kwenye soka. Majaribio hayo ambayo yanafanywa na kampuni Sony ambao ndio wamiliki wa mfumo huo ambao pia hutumika katika mchezo wa tenisi na kriketi, yanajaribiwa katika Uwanja wa St. Mary uliopo jijini Southampton. Mfumo mwingine ambao utafanyiwa majaribio ni wa GoalRef ambao unamilikiwa na kampuni ya Ujerumani, wenyewe utafanyiwa majaribio yake katika michezo ya nchini Denmark. IFAB inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kama teknologia ya mstari wa goli itaweza kutumika viwanjani katika mkutano wake unaotarajiwa kufanyika Julai 2 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment