Sunday, May 13, 2012
MASHABIKI W FERNABAHCE WAFANYA VURUGU UTURUKI.
MAMIA ya mashabiki wa nchini Uturuki walivamia uwanjani na kuanza kugombana na polisi wakati wa mchezo Ligi Kuu ya nchi hiyo kati Galatasaray na mahasimu wao Fernabahce mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bila ya kufungana hivyo kupelekea Galatasaray kutawadhwa mabingwa wapya wa ligi hiyo. Mashabiki wa Fernabahce walivunja viti vya uwanjani na kuanza kuwarushia polisi ambao walikuwa wakitumia ngao walizokuwa nazo kuwakinga wachezaji ambao walikuwa wakielekea katika vyumba vya kubadilishia nguo katika Uwanja wa Sukru Saracoglu. Mara baada ya polisi kuhakikisha wachezaji wako kwenye vyumba vyao vya kubadilishia nguo walilazimika kurusha mabomu ya machozi ili kuwatawanya mashabiki hao. Katika tukio lingine mtu mmoja anayekadiriwa kuwa na miaka 29 ambaye alikuwa amevalia jezi ya timu ya Galatasaray alichomwa kisu tumboni na mashabiki wa Fernabahce ambapo baadae taarifa zilitoka kuwa mtu huyo alikuwa akiendelea vizuri. Wakati mashabiki wa Fernabahce wakiendelea na vurugu hizo kwa upande wa mashabiki wa Galatasayar wao walikuwa katika mitaa huku wakipiga honi magari yao kusherehekea ushindi wa timu yao kunyakuwa taji hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment