Sunday, May 13, 2012
HOSSAM NA IBRAHIM HASSAN WATIMULIWA AL MASRY.
MWENYEKITI wa klabu ya Al Masry, Kamel Abo Ali ameweka wazi kuwa hatawaongeza mkataba viongozi wake wa benchi la ufundi la klabu hiyo Hossam Hassan na Ibrahim Hassan ambao ni mapacha. Ali amesema kuwa matokeo ya kutowaongeza mkataba ndugu hao inatokana na timu hiyo kufungiwa na Chama cha Soka nchini Misri-EFA baada ya vurugu zilizotokea Februari mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 74 na wengine mamia kujeruhiwa. Mwenyekiti huyo aliendelea kusema kuwa Hossam na Ibrahim ni makocha wazuri lakini hawawahitaji katika kipindi hiki ambapo mkataba wao unaishia Julai mwaka huu. Ali pia amesema kuwa klabu hiyo haitawalipa makocha hao mishahara yao ya miezi mitatu iliyopita kwasababu hawakufanya kazi yoyote toka timu hiyo ifungiwe Februari. Klabu hiyo pia aimelazimika kuwapeleka kwa mkopo kwenye timu zingine wachezaji wake haswa wale wenye mikataba mirefu katika kipindi cha majira ya kiangazi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment