MESSI KUMSAIDIA MTOTO WA MIAKA 12.
|
Waleed Kashash |
MTOTO wa miaka 12 ambaye amegundulika na ugonjwa ambao umeshawahi kumsumbua mshambuliaji wa nyota wa Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kupatiwa matibabu ambayo yatakuwa yakilipiwa na nyota huyo mwenye miaka 24. Mtoto huyo aitwaye Waleed Kashash ambaye ni raia wa Morocco aligundulika na ugonjwa ambao unamzuia kukua ambao kitaalamu unaitwa Growth Hormone Deficiency-GHD ambapo mtoto huyo amepania kupambana nao ili hapo baadae aweze kucheza mpira lakini gharama za matibabu hayo ndio zilizokuwa kikwazo kwa mtoto huyo. Hatahivyo mwanamke mmoja aitwaye Soad al-Affani aliamua kumwambia Messi juu ya habari za ugonjwa wa mtoto huyo ambapo nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alijitolea kulipa gharama za matibabu ya mtoto huyo mpaka atapotimiza miaka 18. Messi pia alipiga picha akiwa ameshikilia fulana ya Waleed na kumuandikia ujumbe wa upendo na kumtaka kuwa jasiri katika kipindi hicho kigumu.
No comments:
Post a Comment