KLABU ya Zamalek ya nchini Misri imeondoa tofauti zilizokuwepo katika yao na kocha mkuu wa klabu hiyo Hassan Shehata. Mwenyekiti wa klabu hiyo Mamdouh Abbas alitangaza jana kuwa Shehata bado ni kocha halali wa timu hiyo na hatarajiwi kuachia wadhifa wake huo. Abbas amesema kuwa wamekataa barua ya kujiuzulu aliyowaandikia kocha huyo kwani bado ataendelea kufanya kazi na klabu hiyo na kilichotokea katik siku za karibuni wameshakirekebisha na mambo yako sawa. Shehata aliandika barua ya kujiuzulu baada ya bodi ya klabu hiyo kushindwa kuchukua hatua za haraka juu ya wachezaji wawili wa klabu hiyo ambao ni Ahmed Mido Hossam na Mahmoud Abd Al Razek waliokuwa wamekorofishana na kocha huyo. Ili kumbakisha kocha huyo klabu hiyo imeamua kumtimua Mido na kumshukuru katika kipindi chote ambacho amekuwa sehemu ya timu hiyo huku Razek akitolewa kwa mkopo ambapo sasa timu hiyo inatarajiwa kuanza mazoezi Juni mosi mwaka huu.
Sunday, May 27, 2012
ZAMALEK PICK SHEHATA OVER MIDO.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment