Sunday, May 27, 2012

KILA LA KHERI TWIGA STARS,


 

TIMU ya taifa ya soka ya wanawake Tanzania, Twiga Stars leo inatarajiwa kushuka dimbani kwenye Uwanja wa Addis Ababa, Ethiopia kumenyana na wenyeji Ethiopia katika mechi ya kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa wanawake. Twiga iliyoondoka nchini Alhamisi na msafara wa watu 24 wakiwemo wachezaji, benchi la ufundi na viongozi itacheza na Ethiopia, imepania kufanya vizuri leo, ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu kwenye Fainali hizo za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake -AWC zitakazofanyika Novemba mwaka huu, Equatorial Guinea. Baada ya mechi ya leo, Addis Ababa, timu hizo zitarudiana Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa Ethiopia itakuwa imekata tiketi ya kwenda Equatorial Guinea. Wachezaji waliopo katika kikosi cha Twiga ni Amina Ally, Asha Rashid-nahodha, Esther Chabruma, Ettoe Mlenzi, Evelyn Sekikubo, Fadhila Hamad, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatib, Fatuma Mustafa, Fatuma Omari, Maimuna Said, Mwajuma Abdallah, Mwanahamisi Omari, Mwanaidi Tamba, Mwapewa Mtumwa, Rukia Hamis, Semeni Abeid na Zena Khamis. Kwa upande wa Benchi la Ufundi ni Charles Mkwasa (Kocha Mkuu), Nasra Mohamed (Kocha Msaidizi), Furaha Francis-Meneja wa Timu

No comments:

Post a Comment