BEKI wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Manchester United, Patrice Evra amesema kuwa kocha wa timu taifa ya Uingereza Roy Hodgson amewapa ahueni baada ya kumuacha beki wao mkongwe Rio Ferdinand katika michuano ya Ulaya. Evra ambaye anacheza klabu moja na Ferdinand amesema kuwa ameshangazwa na suala la kuachwa kwa beki huyo kwani mchezaji wa kiwango cha juu na ana uzoefu wa kutosha na michuano mikubwa kama hiyo. Beki aliendelea kusema pengine Ferdinand ana kila sababu ya kusononeshwa na kitendo hicho lakini hata hivyo ni ahueni kwao wakati watapocheza na Uingereza katika mchezo wa ufunguzi katika kundi D kwenye michuano hiyo. Ferdinand mwenye umri wa miaka 33 anaamini kuwa ameondolewa katika kikosi hicho kwasababu angecheza pembeni ya beki wa Chelsea John Terry ambaye ana kesi itakayo mkabili mwezi ujao juu ya tuhuma za ubaguzi dhidi ya mdogo wake Rio aitwae Anton.
Thursday, June 7, 2012
EURO 2012: KUKOSEKANA KWA FERDINAND NI AFADHALI KWETU - EVRA.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment