TIKETI kwa ajili ya mechi za timu ya taifa ya Uingereza katika michuano ya Ulaya zimeshuka bei kutokana na mashabiki wengi wa soka wa nchi hiyo kutokuwa tayari kufunga safari ndefu ya kwenda nchini Ukraine kwa ajili ya kuishuhudia timu yao. Uingereza ni mojawapo ya timu ambazo huwa zinakuwa na mashabiki wengi zaidi katika michuano mikubwa lakini mabadiliko ya hivi karibuni ikiwemo kubadilisha kocha pamoja na majeruhi yanayowasumbua wachezaji wengi nyota imeonyesha kuwakatisha tamaa mashabiki wa nchi hiyo. Bei za tiketi kwa ajili ya mchezo wa ufunguzi utakaochezwa Jumatatu kati ya Uingereza na Ufaransa zimeshuka kwa euro 40 kwa kila tiketi huku tiketi za michezo mingine katika kundi D dhidi ya Sweden na Ukraine na zikiuzwa kwa bei rahisi zaidi. Sio Uingereza pekee ilioathirika na suala kwani pia tiketi za mchezo mkubwa katika kundi B kati ya Uholanzi na Ujerumani na zimeporomoka mpka euro 19 ikilinganishwa na bei iliyoanzia ya euro 30. Bei za tiketi kwa ajili ya mabingwa watetezi wa michuano hiyo Hispania bado zimesimama palepale na mashabiki wengi wameonekana kujitokeza kuzinunua.
No comments:
Post a Comment