Wednesday, June 6, 2012

EURO 2012: UJERUMANI YARUHUSU MITUNGI, SIGARA NA MADEMU KWA WACHEZAJI WAKE.

Nahodha wa Ujerumani Philipp Lahm akikata kilaji na mkewe.
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Ujerumani wameruhusiwa kunywa vileo na kuvuta sigara kwa wale watumiaji wa vitu hivyo pamoja na kutumia simu zao kuingia katika mitandao ya kijamii na kujichanganya na marafiki zao wao kike wakati wa michuano ya Ulaya inayotarajiwa kuanza Ijumaa, huko Poland na Ukraine. Pamoja na madhara yatokanayo na uvutaji wa sigara kocha wa timu hiyo Joachim Low ambaye zamani naye alikuwa akivuta sigara amesema kuwa hawezi kuwafungia wachezaji kufanya hivyo kasoro wakati wa kula na muda wa mkutano. Hata hivyo inaonekana katika kikosi hicho kipa namba mbili Tim Wiese ndio pekee anayevuta sigara katika kikosi hicho cha wachezaji 23. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la kila siku nchini Ujerumani imesema kuwa wachezaji na makocha pia wataruhusiwa kunywa pombe pamoja na mvinyo ikiaminika kuwa watakuwa wakijiheshimu wakati wakitumia vileo hivyo. Mkurugenzi wa timu hiyo Oliver Bierhoff amethibitisha kuwa wake pamoja na watoto wa wachezaji wataruhusiwa kuwatembelea hotelini katika kipindi cha mapumziko baada ya mechi lakini aliongezea kuwa bado hawajaamua kama wataruhusiwa kulala hotelini hapo.

No comments:

Post a Comment