Saturday, July 14, 2012

ANOUMA KUSHINDANA NA HAYATOU CAF.

Jacques Anouma.
 RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka nchini Ivory Coast-FIF, Jacques Anouma ameonyesha nia ya kugombea nafasi ya urais wa Shirikisho la Soka la Afrika-CAF mwaka ujayo, nafasi ambayo kwasasa inashikiliwa na Issa Hayatou. Anouma aliomba FIF imuunge mkono katika nia yake hiyo baada ya kuandika barua kwenda kwa viongozi wa shirikisho hilo lenye makao yake makuu jijini Abidjan kama kanuni za CAF zinavyosema. Taarifa za ndani kutoka katika shirikisho hilo zimesema kuwa wameonyesha nia kumuunga mkono Anouma ambaye pia amesema anasubiria ridhaa kutoka kwa rais wa nchini hiyo Alassane Ouattara. Anouma mwenye umri wa miaka 58 ana taaluma ya uhasibu na pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA na CAF, na amewahi kuwa rais wa Muungano wa Vyama vya Soka vya Afrika Magharibi-WAFU. Katika uchaguzi ambao unatarajiwa kufanyika Machi mwaka 2013 wakati wa Mkutano Mkuu utakaofanyika jijini Morocco, Hayatou anatarajia kutetea kiti chake hicho kwenye uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment