Saturday, July 14, 2012

MAHAKAMA YATENGUA UCHAGUZI WA FA BENIN.


 

SAKATA la uchaguzi wa Shirikisho la Soka nchini Benin limechukua sura mpya baada ya mahakama ya rufani kumtambua Victorian Attolou kama rais wa shirikisho hilo katika uchaguzi uliofanyika Februari mwaka 2011. Uamuzi huo wa mahakama unaenda kinyume na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA na Shirikisho la Soka Afrika-CAF ambao wao walikuwa wakimtambua Anjorin Moucharafou kama kiongozi halali wa shirikisho la nchini hiyo. Mahakama ya rufani ya Cotonou katika taarifa yake ilitoa maamuzi hayo jana na kumtaka Moucharafou kukabidhi madaraka hayo kwa Attolou haraka iwezekanavyo. Mahakama hiyo pia ilifuta uchaguzi mkuu ambao ulimuweka madarakani Moucharafou ambaye alitumikia kifungo cha miezi sita jela baada ya kukutwa na hatia kushindwa kutumia ipasavyo fedha ilizopewa shirikisho hilo na kampuni moja ya simu ya nchi hiyo ingawa baadae mahakama kuu ilimuacha huru baada ya kuona hana hatia.

No comments:

Post a Comment