
Friday, July 6, 2012
ARSENAL YAFUTA ZIARA YA NIGERIA.
KLABU ya Arsenal imefuta ziara yake ya kwenda nchini Nigeria ambapo walipangwa kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya nchi hiyo Super Eagles. Mkurugenzi wa Masoko wa Arsenal, Angus Kinnear amesema kuwa wamefuta mchezo huo umefutwa kutokana na waratibu wa ziara ya timu hiyo kushindwa kufikia matakwa waliyokubaliana. Kinnear aliendelea kusema kuwa kuingiza klabu kubwa kama Arsenal katika soko la kimataifa siku zote lazima kuwe na changamoto zake ndio maana wameamua kufuta ratiba hiyo na kujaribu kupanga ziara nyingine mwaka ujao. Mkurugenzi huyo aliendelea kusema kuwa anatambua uwepo wa mashabiki wengi wa timu hiyo Afrika hususani Nigeria hivyo aliomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza kwa kushindwa kufanya ziara yao hata hivyo ameahidi kuwa watajitahidi mwakani waweze kwenda huko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment