Sunday, July 15, 2012

AYEW APONA BEGA.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ghana na klabu ya Olympique de Marseille ya Ufaransa, Andre Ayew ametanabaisha kuwa maumivu ya bega yaliokuwa yakimsumbua kwa kipindi kirefu sasa yameanza kutoweka. Ayew alipata maumivu hayo ya bega wakati akiiwakilisha nchi yake katika michuano ya Mataifa ya Afrika iliyofanyika mapema mwaka huu lakini alimua kukataa kufanyiwa upasuaji. Baada ya kukataa hatimaye alikuja kukubali kufanyiwa upasuaji April 24 na alitegemewa kukaa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu ingawa hata hivyo alikuwamo katika kikosi cha timu yake kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Benfica ambapo Marseille walifungwa mabao 2-0. Alikaririwa katika mtandao wa klabu hiyo akidai kuwa bega lake linaendelea vyema nay ale maumivu ambayo alikuwa akiyasikia mwanzoni yametoweka kabisa.

No comments:

Post a Comment