![]() |
Reinhard Rauball. |
Rais wa Bungesliga, Reinhard Rauball amesema kuwa Blatter anapaswa kujiuzulu wadhfa wake haraka iwezekanavyo ili shirikisho hilo liweze kujipanga upya. Kauli ya Rauball imekuja kufuatia Blatter kukubali kufahamu suala la malipo yaliyofanywa na kampuni ya masoko ya ISL kwenda kwa rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange lakini akasisitiza kuwa yalikuwa ni malipo halali katika kipindi hicho cha miaka ya tisini. Blatter aliendela kusema kuwa watu wengi wamekuwa wakimshinikiza ajiuzulu kutokana na kupokea mlungula kitu ambacho Mahakama Kuu ya Shirikisho nchini Switzerland imeshindwa kumtia hatiani kutokana na tuhuma hizo. Rauball pia alitaka FIFA kuitisha mkutano wa dharura ambao wajumbe wake watatakiwa kumvua urais wa heshima Havelange kutokana na tuhuma zinazomkabili.
No comments:
Post a Comment