Sunday, July 15, 2012

KHANA ADUNDWA TENA MAREKANI.

Amir Khan.
BONDIA Amir Khan wa Uingereza wa Uingereza amepata kipigo cha pili mfululizo baada ya kusimamishwa katika raundi ya nne na bondia ambaye hajawahi kupigwa Danny Garcia katika pambano lililofanyika jijini Las Vegas jana usiku. Khan alijikuta akiangushwa chini mara tatu katika pambano hilo hivyo kumfanya Garcia kutetea mkanda wake wa WBC kumpokonya Khan mkanda wake wa WBA uzito wa light-welter. Baada ya kuanza vizuri pambano hilo Khan alijikuta akipata kipigo katika raundi ya tatu kilichompeleka chini na hakuweza tena kurudi mchezoni baada ya kipigo hicho mpaka kujikuta akipoteza pambano hilo katika raundi ya nne. Akihojiwa mara baada ya pambano hilo Khan amesema kuwa alifanya makosa kidogo kwenye pambano hilo na Garcia akatumia udhaifu huo kumtandika na kusikitika kwamba huo haukuwa usiku wake lakini amejifunza kutokana na kipigo hicho. Hicho kinakuwa kipigo cha tatu kwa Khan na ambacho kimekuja baada ya kupoteza pambano dhidi ya Lamont Peterson ambaye alimpiga katika pambano lililoamuliwa kwa utata Desemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment