Mourinho. |
KLABU ya Barcelona imechukizwa na uamuzi wa Shirikisho la Soka nchini Hispania-RFEF wa kumfutia adhabu ya kufungiwa mechi mbili kocha wa Real Madrid Jose Mourinho kwa kumtoboa na kidole jichoni kocha msaidizi wa Barcelona Tito Vilanova msimu uliopita. Ikiwa umebaki mwezi mmoja kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu nchini maarufu kama La Liga tayari uadui kati ya timu hizo mahasimu umeshaanza kujitokeza. Msemaji wa Barcelona Toni Freixa amesema kuwa uamuzi uliofanywa na RFEF kuhusiana na sula la Mourinho unalitia doa shirikisho hilo na litakuwa linachochea matukio kama hayo kuendelea kutokea. Freixa aliendelea kusema kuwa uamuzi huo haumaanishi kwamba mtuhumiwa hakufanya kitendo hicho lakini utakuwa ni kichocheo cha watu wenye tabia kama hizo kuendelea kuzifanya kwakuwa wanajua hataweza kuadhibiwa. Mourinho alimtoboa kidole kwa nyuma Vilanova wakati wa mchezo baina ya timu hizo zilipokutana katika Kombe la Mfalme na kufungiwa michezo miwili lakini rais wa RFEF Angel Maria Villar alitengua adhabu hiyo baada ya kuteuliwa tena kushikilia wadhfa huo katika kipindi cha miaka saba mingine.
No comments:
Post a Comment