Wednesday, July 11, 2012

URUGUAY YAPATA KOCHA MPYA.

Gerardo Pelusso.
TIMU ya taifa ya Uruguay ambayo iko katika hatihati ya kushindwa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia itakalofanyika Brazil mwaka 2014 wamepata kocha mpya aitwaye Gerardo Pelusso ambaye atachukua nafasi ya kocha Francisco Arce aliyetimuliwa. Arce ambaye alikuwa nahodha wa zamani wa kikosi hicho katika michuano ya Kombe la Dunia alitimuliwa baada ya matokeo mabaya ya kikosi hicho yaliyopelekea timu hiyo kushika nafasi ya pili kutoka mwisho katika msimamo wa kundi la timu za Amerika Kusini. Pelusso mwenye umri wa miaka 58 ambaye alikuwa akifundisha klabu ya Ligi Daraja la kwanza nchini humo ya Olimpia alikabidhiwa mikoba hiyo kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu wa ligi ya ndani. Rais wa Chama cha Soka cha nchini hiyo-APF, Juan Angel Napout alithibisha uteuzi huo na kusema kuwa walikuwa wakihitaji kocha mwenye uzoefu wa aina yake ili ajaribu kuivusha timu hiyo ishiriki michuano ya Kombe la Dunia ijayo. Baada ya Paraguay kuvuna alama nne katika michezo mitano waliyocheza Pelusso atakuwa na kibarua kigumu pale atakapokutana na Argentina ugenini Septemba 7 mwaka huu kabla ya kuwakaribisha Venezuela siku nne baadae.

No comments:

Post a Comment