MARADONA ATIMULIWA AL WASL.
 |
Maradona. |
NAHODHA wa zamani wa kimataifa wa Argentina ambaye alikiongoa kikosi hicho kunyakuwa michuano Kombe la Dunia mwaka 1986, Diego Maradona ametimuliwa kufundisha klabu ya Al Wasl ya Muungano wa Falme za Kiarabu-UAE. Maradona mwenye umri wa miaka 51, ambaye alikubali kusaini mktaba wa kuinoa klabu hiyo kwa miaka miwili alitimuliwa baada ya kikao cha bodi kilichokutana jana. Taarifa ya klabu hiyo iliyotumwa katika mtandao imesema kuwa katika kikao hicho ambacho bodi ya wakurugenzi wa klabu hiyo walikutana waliazimia kumuondoa Maradona pamoja na benchi lote la ufundi la klabu hiyo ili kupanga safu nyingine mpya. Tetesi juu kuondoka kwa Maradona zilianza kufuatia aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo Marwan bin Bayat ambaye ndiye alikuwa akimuunga mkono kocha huyo kujiuzulu wadhfa wake huo na nafasi yake kuchukuliwa na mtu mwingine Juni mwaka huu. Hata hivyo baada ya mkutano wa kwanza wa bodi mpya uliofanyika mwezi uliopita mwenyekiti wake Dr Mohammed Ahmad bin Fahad alikaririwa akisema kuwa maradona ataendelea kuwa kocha wa klabu hiyo kwa msimu ujao na hakutakuwa na mabadiliko katika nafasi yake.
No comments:
Post a Comment