BLATTER ATAKA HAVELANGE AVULIWE URAIS WA HESHIMA.
 |
Joao Havelange. |
RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Sepp Blatter amesema kuwa aliyekuwa rais wa zamani wa shirikisho hilo Joao Havelange anatakiwa kuvuliwa wadhfa wa urais wa heshima aliopewa kutokana na tuhuma za rushwa katika kipindi chake cha uongozi zinazomkabili. Kauli ya Blatter inakuwa inaenda kinyume akiwa kama rais wa FIFA, kwani katika mkutano wa shirikisho hilo uliofanyika nchini Hungary Mei mwaka huu alisimama kumtetea Havelange mwenye umri wa miaka 96 ambaye kwasasa ni mgonjwa. Lakini Blatter amekuwa katika msukumo mkubwa toka wili iliyopita baada ya FIFA kuitangaza taarifa ya waendesha mashitaka nchini Switzerland iliyoezea kwamba Havelange alikubali mlungula kutoka kwa kampuni ambayo ni wakala wa masoko ya ISL katika miaka ya tisini. Akikaririwa na gazeti moja la kila siku nchini humo Blatter amesema kuwa Havelange lazima avuliwe wadhfa huo kutokana na tuhuma hizo zinazomkabili sasa. Blatter alikuwa mmoja wa viongozi wa juu wakati Havelange akiwa rais wa FIFA kabla ya kuchaguliwa kuchukua kiti cha Havelange mwaka 1998.
No comments:
Post a Comment