Monday, July 16, 2012

SINA URAFIKI NA PEREZ - ROSELL.

Sandro Rosell.
RAIS wa klabu ya Barcelona, Sandro Rosell amekiri wazi katika mahojiano nchini Hispania kuwa hana urafiki wowote na rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez ambao ni mahasimu wao wa kubwa katika Ligi Kuu nchini Hispania inayojulikana kama La Liga. Hiyo siyo mara ya kwanza kwa Rosell kutoa kauli zenye utata wiki hii baada ya kukaririwa akiponda La Liga msimu uliopita Mbapo Barcelona ilimaliza katika nafasi ya pili mbele ya mahasimu wao Madrid. Rosell mwenye umri wa miaka 48 alithibitisha kuwa klabu hiyo haitabadilisha aina ya mchezo wanaocheza sasa pamoja na kukosa taji la La Liga msimu uliopita ambalo lilichukuliwa na Madrid. Rais huyo pia alizungumzia uhasama baina ya klabu hizo mbili na kudai kuwa mpaka sasa mekuwa akisikia kuwa kuna uhasama lakini hajapata taarifa zozote kuhusiana na hilo na kutakuwepo na matatizo kama hayo itawajibika kuyashughulikia na kuweka sawa.

No comments:

Post a Comment