WANAMICHEZO WOTE KUPIMWA KABLA NA BAADA YA OLIMPIKI.
 |
Dwain Chambers. |
KATIKA michuano ya Olimpiki inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu jijini London, Uingereza itashuhudia operesheni ya kihistoria ya kupambana na madawa yaliyokatazwa michezoni. Karibu nusu ya washiriki wote wanatarajiwa kufanyiwa vipimo ili kujua kama watakuwa wametumia madawa hayo huku kukiwa na madaktari wapatao 150 watakaochukua vipimo 6,000 kuanzia sasa na mwishoni mwa mashindano ya Paralimpiki. Kila mwanariadha atakayeshinda medali katika michuano hiyo yote miwili atachukuliwa vipimo hivyo. Muongeleaji mlemavu anayeshiriki paralimpiki, Graham Edmunds ana matumaini na kila kitu kinachofanyika sasa ili kuwabaini wanamichezo wanaodanganya kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu na kuifanya michuano hiyo iwe na maalumu nay a kupendeza. Katika michuano hiyo mkimbiaji wa mbio fupi Dwain Chambers na muendesha baiskeli David Millar wanatarajiwa kushiriki michuano hiyo baada ya Chama cha Olimpiki cha Uingereza kuwafungia maisha kutokana na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu lakini walipunguziwa na adhabu na kuachiwa huru na Mahakama ya Michezo ya Usuluhishi ya Kimataifa baada ya kukata rufani.
No comments:
Post a Comment