Sunday, July 8, 2012

I WON'T CHANGE THE WAY I OPARATES THE CLUB - WENGER.

Arsene Wenger.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesisitiza kuwa hawezi kubadilisha mfumo anaoendesha klabu hiyo hata kama wachezaji wake nyota wataendelea kuondoka. Wenger na bodi ya klabu hiyo walikuwa katika wakati mgumu juu ya uamuzi wa mshambuliaji wake nyota Robin van Parsie kuondoka klabuni hapo kwasababu haoni kama timu inaweza kunyakuwa mataji. Lakini Wenger ameonekana akifuata maneno ya nguli wa soka Johan Cruyff ambaye anaamini kuwa timu yoyote inaweza kushinda michuano ya Klabu Bingwa ya Ulaya bila ya kutumia fedha nyingi katika usajili. Cruyff anaamini kuwa timu inaweza kupata mafanikio kwa kutumia wachezaji vijana na wenye vipaji ambapo suala hilo linaungwa mkono na Wenger ambaye amesema hawezi kubadilisha aina yake hiyo ya kutumia wachezaji makinda. Wenger amekiri kuwa muda mwingine kazi yake kubwa ya kuwapika vijana imekuwa ikivurugwa na wengine baada ya kuwapoteza nyota wake kama Samir Nasri, Gael Clichy na Cesc Fabregas katika kipindi ambacho ndio walitakiwa kuiletea vikombe klabu hiyo lakini hajakata tama na hilo. Juhudi za Wenger kumbakisha Van Persie kwa kuwasajili Lukas Podolski na Olivier Giroud kwa jumla ya paundi milioni 24 zimeonekana kugonga mwamba wa kumshawishi mshambuliaji kuongeza mkataba wake ambao unamalizika Juni mwakani.

No comments:

Post a Comment