| Zola. |
MSHAMBULIAJI wa zamani wa kimataifa wa Italia na klabu ya Chelsea, Gianfranco Zola amesaini mkataba wa miaka miwili wa kuinoa klabu ya daraja la pili ya Watford. Mkurugenzi wa Ufundi wa klabu hiyo Gianluca Nani alithibisha timu hiyo kuingia mkataba na kocha huyo na kusema kuwa kila mtu anajua jinsi gani Zola livyo na mapenzi na mchezo wa soka. Nani alindelea kusema kuwa mashabiki wa klabu hiyo wategemee kikosi kitakachokuw kikishambulia kwa aina yake wakati kitakapokuwa chini ya kocha huyo katika kipindi hicho. Zola ana uzoefu wa kutosha na soka la Uingereza baada ya kucheza kwa mafanikio kwa miaka saba akiwa na Chelsea kabla ya kuwa meneja wa klabu ya West Ham United kwa kipindi kifupi.
No comments:
Post a Comment