BINGWA ngumi wa dunia wa uzito wa juu Wladimir Klitschko amefanikiwa kutetea mikanda yake ya WBA, IBF na WBO baada ya kumchakaza Tony Thompson wa Marekani katika raundi ya sita. Klitschko ambaye ni raia wa Ukraine amefanikiwa kuongeza rekodi yake ya kutopigwa kwa miaka nane sasa wakati alipompiga Thompson katika pambano lililofanyika jijini Berne, Switzerland jana. Huo ni pambano la 58 kwa bondia huyo mwenye umri wa miaka 36 ambapo mapambano 51 kati ya hayo ameshinda knockout akiwa amepoteza mapambano matatu pekee. Wladimir na kaka yake Vitali wamekuwa wakitamba katika ngumi za uzito wa juu kwa miaka mingi sasa mpaka inabidi kurudiana na mabondia ambao wamekwishawahi kucheza nao kipindi cha nyuma. Thompson ambaye ana umri wa miaka 40 mara ya mwisho alipambana na Wladimir mwaka 2008 ambapo mmarekani alichapwa katika raundi ya 11.

Sunday, July 8, 2012
WLADIMIR KLITSCHKO ATETEA MIKANDA YAKE.

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment